Mkurugenzi Mtendaji wa ELISHA FASHION AND DESIGN YOUTH SUPPORT FOUNDATION (EFAD) Ndugu Elisha W. Shombe akitoa salamu za EFAD
Mkurugenzi Mtendaji wa ELISHA FASHION AND DESIGN YOUTH SUPPORT FOUNDATION (EFAD) Ndugu Elisha W. Shombe akitoa salamu za EFAD
Mkurugenzi Mtendaji wa ELISHA FASHION AND DESIGN YOUTH SUPPORT FOUNDATION (EFAD) Ndugu Elisha W. Shombe akitoa salamu za EFAD kwa wakufunzi wa mafunzo ya siku mbili yaliyotolewa na shirika la Foundation for Civil Society (FCS). Mafunzo yaliyofadhiriwa na UNICEF, yaliyolenga kujengea uwezo asasi changa, hasa, katika maeneo ya utendaji, usimamizi wa sera, utawala wa fedha, n.k. ili kuwanufaisha watoto na vijana.
Katika salamu zake, Mkurugenzi wa EFAD, ndugu Elisha Shombe, alipata wasaa wa kuelezea maono, Shabaha na Malengo ya shirika hilo, lenye lengo kuu la kuwajengea uwezo vijana na watoto waishio katika mazingira magumu.
Ndugu Shombe alisema, kuwa kiu ya shirika ni kuwasaidia vijana tajwa kwa kuwapa ujuzi wa elimu ya ushonaji na ubunifu wa mavazi, ili kuwategemeza katika kujenga uchumi wa Taifa. Vilevile, kwa upande wa watoto, lengo kuu la asasi ya EFAD ni kuwawezesha watoto waliopo mashuleni kwa dhana na vifaa vya kitaaluma, kama sare za shule na chakula.
Kwa mtazamo wake, ndugu Shombe, anabainisha kuwa, mafunzo haya yamekuja katika wakati muafaka, na yameendana na kiu ya asasi ya EFAD, katika kuisaidia jamii. Hii ni kutokana na elimu haba ya uandishi wa miradi iliyokuwa ikiikabili asasi hii.
Vilevile, ndugu Shombe alibainisha kuwa, mafunzo hayo, yatasadia kuandika mradi ambao, unaweza kusaidia upatikanaji wa vifaa vya ushonaji na bajeti ya uendeshaji ili kuwafikia watoto wengi zaidi na vijana pomoni waishio katika mazingira magumu, ndani na nje ya mkoa wa Songwe.