MKUU WA WILYA YA MBOZI AWAPONGEZA EFAD
MKUU WA WILYA YA MBOZI AWAPONGEZA EFAD
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe. Hamad Mbega(Wa kwanza Kutoka kushoto), pongezi hizo ni wakati alipofanya ziara katika ofisi za NGO hiyo zilizopo Nselewa Mkabala na Ofisi za Mamlaka ya Mapato Songwe(TRA). Mhe. mbega amesema wao kama serikali wanatambua mchango wa Elisha youth foundation katika kutatua changamoto za kijamii, hata hivyo ametumia nafasi hiyo kuiomba EFAD kusaidia katika kukabiliana na uhaba wa madawati 12,000 katika shule za halmashauri ya wilaya ya mbozi kwa shule za msingi na sekondari.
Naye Mkurugenzi wa EFAD Elisha Shombe(Wa Pili Kutoka Kushoto) amesema wamelipokea ombi la Mkuu wa Wilaya ya Mbozi na kuwa wataliwasilisha kwa wadau wa Maendeleo ili waweze kulifanyia kazi pale watakapojaliwa.