Waangalizi wa Uchaguzi wa EFAD Wapewa Mafunzo na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jijini Dodoma
Waangalizi wa Uchaguzi wa EFAD Wapewa Mafunzo na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jijini Dodoma
Pichani ni waangalizi wa uchaguzi kutoka shirika lisilo la kiserikali EFAD (Elisha Fashion & Design Youth Support Foundation) wakiongozwa na Mkurugenzi wa EFAD, Elisha Shombe (kushoto) na Mratibu wa shirika hilo, Omary Kaita (kulia), wakiwa katika semina maalumu ya mafunzo iliyoandaliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) jijini Dodoma, ndani ya ukumbi wa Jiji Mtumba.
Mafunzo hayo yamelenga kutoa miongozo, taratibu na maadili ya uangalizi wa uchaguzi, ili kuhakikisha kuwa waangalizi wote wanafanya kazi zao kwa kuzingatia misingi ya uwazi, haki na kutokuwamo kwa upendeleo katika mchakato mzima wa uchaguzi.
Mafunzo kama haya ni sehemu ya jitihada za EFAD katika kukuza ushiriki wa wananchi na kuhimiza uwajibikaji katika michakato ya kitaifa, hasa uchaguzi.
Timu ya wajumbe kutoka shirika la EFAD wakiwa kwenye maeneo ya vituo kupigia kura wakati wa uchaguzi oktoba 29 2025 wakitekeleza wajibu wao kama waangalizi wa ndani katika uangalizi wa Uchaguzi Mkuu