ELISHA FASHION AND DESIGN SONGWE EXPO
ELISHA FASHION AND DESIGN SONGWE EXPO
Elisha Fashion and Design Youth Support Foundation (EFAD) ilishiriki maonesho ya wajasiriamali mkoani Songwe, ambapo ilionesha bidhaa mbalimbali za ubunifu zinazotengenezwa kupitia programu zake za mafunzo kwa vijana.
Picha zinaonesha bidhaa hizo, pamoja na Mkurugenzi wa EFAD akiwa na wananchi waliofika kutembelea banda, wakipata maelezo kuhusu namna tunavyowawezesha vijana kupata ujuzi na kujiajiri kupitia ubunifu.
Ushiriki huu ulitoa fursa ya kutangaza kazi za vijana, kuonesha uwezo wao, na kuimarisha dhamira ya EFAD ya kuwajengea vijana msingi wa kujitegemea kiuchumi.
Mkurugenzi wa EFAD, Ndugu Elisha Shombe, akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa Mhe. Jabir Omary Makame Mkuu wa Mkoa wa Songwe kama utambuzi wa mchango wa shirika katika maonesho ya wajasiriamali Mkoa wa Songwe