EFAD YASHIRIKI MAFUNZO YA SIKU MBILI YA KUJENGEWA UWEZO WA KIUTENDAJI.
EFAD YASHIRIKI MAFUNZO YA SIKU MBILI YA KUJENGEWA UWEZO WA KIUTENDAJI.
Shirika lisilo la Kiserikali la ELISHA FASHION AND DESIGN YOUTH SUPPORT FOUNDATION (EFAD) Limebahatika kuwa miongoni mwa Mashirika 30, nchini Tanzania, kupewa mafunzo ya kujengewa uwezo wa kiutendaji kwa manufaa ya wahitaji wa Tanzania, hasa, watoto na vijana wenye umri wa miaka kati ya 10 hadi 19.
Mafunzo hayo yaliyotolewa na Shirika la FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY (FCS) kwa kushirikiana na Shirika la Watoto Ulimwenguni UNICEF, yallilenga kuwezesha mashirika machanga, kama EFAD, kwa kuwajengea uwezo wa kiutendaji, hasa Katika maeneo ya usimamizi wa miradi, usimamizi wa rasilimali fedha, utawala bora, mambo mengine ni, mafunzo ya sera za faragha n.k